1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Shambulizi limeua polisi 25 nchini Irak

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Bc

Hadi askari polisi 25 wameuawa nchini Irak katika shambulizi lililofanywa mji wa Bakuba,kiasi ya kilomita 60 kaskazini-mashariki ya mji mkuu Baghdad.Zaidi ya watu 15 wengine pia wamejeruhiwa baada ya mshambulizi aliejitolea maisha muhanga kujiripua mbele ya makao makuu ya polisi ambako polisi walikuwa wakingojea kuingia ndani kuhudhuria mafunzo ya kila siku.