1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wahukumiwa kifo.

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoe

Mahakama maalum mjini Baghdad imewahukumu adhabu ya kifo watu watatu, ikiwa ni pamoja na binamu yake Saddam Hussein , anayejulikana kwa jina la Chemical Ali. Ali Hassan al-Majid alisimama kimya wakati jaji akisoma hukumu yake ya kifo kwa kunyongwa kwa madai kadha ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki dhidi ya Wakurdi wa Iraq. Wakurdi upande wa kaskazini wa Iraq walishangilia hukumu hiyo ya kifo aliyopewa Majid ambaye alikuwa akionekana kuwa msanifu wa kampeni hiyo iliyofanyika katika mji wa Anfal, ambapo zaidi ya raia wa Kikurdi 180,000 wanaaminika kuwa wameuwawa.

Wajumbe wengi wa ngazi ya juu wa zamani katika utawala wa Saddam Hussein pia wamepewa adhabu ya kifo, na wengine wawili wamepewa adhabu ya kifungo cha maisha jela wakati mtu wa sita ameachiliwa huru.