1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanajeshi sita wa Marekani wauwawa

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLq

Wanajeshi sita wa Marekani wameuwawa kwenye mripuko wa bomu kaskazini mwa Irak leo asubuhi.

Wanajeshi hao walikuwa wakisafiri kwenye msafara katika mkoa wa Salahuddin wakati bomu liliporipuka karibu na magari yao. Wanajeshi wengine watatu wamejeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo.

Hapo jana, bomu lilikuwa limetegwa ndani ya motokaa liliripuka na kuwaua watu takriban 30 na kuwajeruhi wengine 65 kwenye wilaya ya kihistoria yenye maduka ya kuuza vitabu mjini Baghdad.