1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanamgambo 13 wauwawa

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYK

Wanamgambo 13 wameuwawa leo kaskazini mwa Baghdad kwenye mapambano makali yaliyozuka wakati vikosi vya Marekani vilipokuwa vikijaribu kumtia mbaroni kiongozi wa kundi la al-Qaeda mjini humo.

Jeshi la Marekani lilitangaza mwanzoni mwa wiki hii kuanza kwa harakati kubwa mpya nchini Irak inayowalenga wanamgambo wa kishia na wa kundi la al-Qaeda.

Wanamgambo hao wanahofiwa huenda wakaongeza mashambulio yao dhidi ya vikosi vya Marekani, wanajeshi wa Irak na raia wa kawaida huku ripoti kuhusu vita vya Irak ikikaribia kuwasilishwa katika bunge la Marekani mwezi ujao.