1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu 58 wauwawa kwa bomu.

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC60

Kiasi watu 58 wameuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika mji wa kati nchini Iraq wa Karbala.

Mlipuko huo ulitokea katika eneo la kibiashara lililokuwa na watu wengi karibu na jengo la ibada la Imam Hussein wakati waumini walipokuwa wakikusanyika kwa ajili ya swala ya jioni.

Hilo ni moja kati ya maeneo matakatifu kabisa ya ibada nchini Iraq. Kufuatia shambulio hilo, watu ambao walikuwapo sehemu hiyo wakiwa na hasira walianza kurusha mawe kwa polisi, wakiwashutumu kwa kushindwa kuwalinda.

Wakati huo huo , wanajeshi wengine tisa wa Marekani wameuwawa nchini Iraq katika muda wa saa 48 zilizopita. Taarifa ya jeshi la Marekani imesema kuwa wanajeshi wanne waliuwawa kwa bomu lililotegwa kando ya barabara katika shambulio kusini mwa Baghdad, wakati wengine watano waliuwawa katika mapambano katika jimbo la Anbar.