1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Watu 80 wauwawa na 150 kujeruhiwa

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSp

Mashambulizi kadhaa ya mabomu katika maeneo mashuhuri ya sokoni ya Washia mjini Baghdad yameuwa takriban watu 80 na kujeruhi wengine zaidi ya 150.

Afisa wa ulinzi amesema mripuko wa bomu lililotegwa kwenye gari kwenye sehemu ya kuegeshea magari chini ya soko la jumla katika wilaya ya Shorja umeuwa zaidi ya watu 30 na kujeruhi wengine 77 wakati moto mkali ulipoteketeza vibanda kadhaa vya nguo.Ameongeza kusema kwamba mripuko mwengine umetokea kwenye Soko la Haraj kama kilomita moja kutoka mahala kulikotokea mripuko wa kwanza na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine zaidi ya 30.

Wakati huo huo mahkama kuu ya Iraq imepitisha hukumu ya kunyongwa kwa makamo wa zamani wa rais Saddam Hussein.Taha Yassin Ramadhan amehukumiwa adhabu ya kifo kwa dhima yake katika mauaji ya Washia 148 kutoka mji wa Dujail hapo mwaka 1980.