1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu kiasi ya 40 wauawa katika machafuko nchini Irak

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2Q

Watu kiasi ya 31 wameuawa nchini Irak katika machafuko ya kidini katika mji wa Balad umbali wa kilomita kama 80 hivi kaskazini mwa mji mkuu Baghdad. Kwa upande mwingine, kumetokea mashambulizi kadhaa ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari katika mji wa Kirkuk kaskazini mwa Irak na kuwauwa kwa uchache watu 8 na kuwajeruhi wengine kiasi ya 10. Mapema ya hapo, watu 6 waliuawa katika mji mkuu Baghdad wakati mabomu mawili yaliporipuliwa kwa kuvizia msafara wa magari ya afisa moja mkuu wa wizara ya mambo ya ndani. Jumamosi, wanajeshi watano wa Marekani waliuawa katika mripuko wa bomu lililotegwa kando na barabara kusini mwa Baghdad.

Takriban wanajeshi 50 kutoka Marekani wameshauawa mnamo mwezi huu pekee nchini Irak. Hayo yakiarifiwa, serikali ya Irak imeahirisha kongamano la kutafuta maridhiano ya taifa na ambalo lilikuwa muhimu katika juhudi za kuusuluhisha mzozo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo. Serikali imesema kuna sababu za dharura ambazo zimepelekea kubatilisha mkutano huo na kwamba utafanyika jumamosi wiki hii. Mkutano huo unatarajia kutafuta mwafaka kati ya wasuni waliowachache na washiha waliowengi kwa lengo la kufikia makubaliano ya kisiasa.