1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu saba wauwawa kwa bomu.

24 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgO

Katika shambulio jingine la kujitoa muhanga nchini Iraq, mshambuliaji amewauwa watu saba ikiwa ni wafanyakazi wa kituo cha polisi mjini Muqdadiya.

Mji huo uko kilometa 90 kaskazini mashariki ya Baghdad. Polisi wamesema kuwa watu wengine 30 wamejeruhiwa.

Mlipuko huo ulifuatiwa na milio kadha ya makombora.

Muqdadiya uko katika jimbo la Diyala, ambalo linamchanganyiko wa Washia na Wasunni.

Nusu saa baadaye , mabomu mawili yaliyotegwa kando ya barabara yalilipuka katika mji wa Khanaqin, na kuwajeruhi raia 18, kwa mujibu wa polisi.