1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu takriban 50 wauwawa

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBf6

Watu takriban 50 wameuwawa kwenye mashambulio ya mabomu yaliyokuwa yametegwa ndani ya magari mjini Bagdad nchini Irak.

Mashambulio hayo yaliwalenga Wairak waliokuwa wakisherehekea ushindi wa timu yao ya taifa ya kandanda katika mchuano wa nusu fainali ambapo iliishinda Korea Kusini kwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti.

Watu wengine takriban 136 wamejeruhiwa kwenye milipuko hiyo iliyotokea magharibi mwa kitongoji cha Mansour na wilaya ya mashariki ya Ghadeer.

Irak itachuana na Saudi Arabia kwenye fainali ya kuwania kombe la Asia Jumapili ijayo mjini Jakarta nchini Indonesia.