1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu tisa wauwawa katika mlipuko.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBu0

Polisi kaskazini magharibi ya Iraq wamesema kuwa mtu aliyejitoa muhanga akiwa katika lori ameuwa watu tisa kwa kuligonga gari hilo katika kituo cha polisi katika mji wa Rabea, karibu na mpaka wa Iraq na Syria.

Lori hilo lilikuwa limewekwa milipuko.

Mlipuko huo pia umewajeruhi watu wengine 22.

Mtu mwingine aliyejilipua alijaribu kushambulia kituo cha upekuzi cha polisi karibu na ramadi, magharibi ya mji mkuu Baghdad.

Kiasi watu sita wamejeruhiwa.

Mjini Falluja , polisi wanasema kuwa wamegundua miili ya watu watano ambao walitekwa nyara siku tatu zilzopita .

Wote wameteswa kabla ya kupigwa risasi.

Jeshi la Marekani limesema kuwa wanajeshi wake wanaofanya doria ya pamoja na wanajeshi wa Iraq wamewakamata watu 16 wanaotuhumiwa kuwa ni wapiganaji wakati wa msako katika kitongoji cha mji wa Baghdad cha Sadr City.