1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Irak kufunga mipaka kati yake na Syria na Iran

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSR

Serikali ya Irak imesema kwamba itafunga mipaka kati yake na Syria na Iran kwa saa 72 na pia kuongeza muda wa amri ya kutotoka nje saa za usiku katika mji wa Baghdad, chini ya mpango wa usalama unaosimamiwa na Marekani na wenye lengo la kudhibiti hali ya usalama katika mji huo mkuu nchini Irak.

Hata hivyo watu 16 wameuwawa na wengine 45 wamejeruhiwa katika mji wa Baghdad wakati gari lililo egeshwa kando ya chuo kimoja cha elimu cha kibinafsi kulipuka magharibi mwa mji wa Baghdad na kusababisha maafa hayo.

Wakati huo huo kikosi maalum cha wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani kinaendelea na uchunguzi wake juu ya raia wawili wa Ujerumani waliotoweka nchini Irak.