1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Kamanda adai kuna sababu zinazoleta matumaini Iraq.

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHc

Kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Iraq, Jenerali David Petraeus, amesema kuwa kuna sababu ya kuwa na matumaini juu ya hatua za hivi sasa za usalama.

Akizungumza katika mahojiano ya televisheni, Petraeus amesema kumekuwa na mashambulio machache ya kimadhehebu mjini Baghdad, tangu wanajeshi zaidi ya 20,000 wa Marekani kuanza kuwekwa katika mji huo wiki chache zilizopita.

Hata hivyo ghasia zimekuwa zikiendelea.

Wanajeshi wanne wa Marekani wameuwawa baada ya kikosi chao kushambuliwa kwa bomu lililokuwa limetegwa barabarani na baadaye kushambuliwa kwa risasi.

Katika shambulio tofauti la bomu lililotegwa barabarani katika mji huo mkuu, polisi wawili wa Iraq wameuwawa na wengine watano wamejeruhiwa.