1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Maafisa wa Iraq na Marekani wazozana juu ya shambulio lililowauwa watu 20

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClB

Maafisa wa Iraq na Marekani wanazozana juu ya mashambulio ya angani yaliyofanyika usiku ambapo watu zaidi ya 20 waliuwawa.

Wanajeshi wa Marekani wanadai katika shambulio hilo wamewauwa wapiganaji 20 wa kundi la kigaidi la al Qaeda wakiwemo wanawake wawili kwenye eneo linalokaliwa zaidi na waasi wa kisunni.

Hata hivyo polisi pamoja na maafisa wa nchini Iraq wanasema waliouwawa kwenye shambulio hilo zaidi ni raia wakiwemo wanawake sita na watoto watano.

Kwingineko zaidi ya wanajeshi 1000 wadenmark na Uingereza wamevamia nyumba kadhaa kusini mwa mji wa Basra na kuwakamata washukiwa watano wanaodaiwa kuhusika katika kuwashambulia wanajeshi.Kwa mujibu wa kikosi cha Uingereza uvamizi huo ndio mkubwa wa aina yake kuwahi kufanyika kusini mwa Iraq.