1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Mabomu zaidi yaripuka nchini Iraq.

31 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxR

Mfululizo wa miripuko ya mabomu kwenye mji mkuu wa Iraq, Baghdad umeuwa watu kiasi ya 36.

Mamlaka ya nchi hiyo imesema bomu lililoripuka katika uwanja uliokuwa na msongamano wa watu lilipelekea vifo vya watu 26 na wengine 60 kujeruhiwa.

Kiasi ya watu kumi waliuwawa katika mashambulizi mengine matano katika maeneo mengine mjini Baghdad.

Wakati huo huo bomu la katika gari limewauwa watu watatu na kuwajeruhi wengine watano katika mji mkuu Baghdad kwenye mji wa Sadr mapema leo asubuhi, ikiwa ni siku moja tu baada ya kuripuliwa bomu lililowauwa watu 33 katika kijiji cha Washia.

Bomu hilo liliripuka licha ya uangalizi mkubwa katika vituo vya ukaguzi katika mji wa Sadr katika maeneo ambayo ni ngome kuu kwa wanamgambo wa Mahdi wanaomtii kiongozi wao muqtada al-Sadr.

Nalo jeshi la Marekani limetangaza kuongezeka kwa vifo vya wanajeshi wake na kufikia 103 katika mwezi huu wa October.