1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Utekaji nyara bado washuhudiwa Iraq

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCib

Visa vya utekaji nyara mjini Baghdad vinazidi kushuhudiwa.Hapo jana watu wasiojulikana wakiwa na bunduki walivamia afisi za shirika la hilali nyekundu linalotoa msaada huko Baghdad na kuwateka nyara watu 28 ikiwa ni pamoja na wafanyikazi wa shirika hilo,wageni na walinzi.

Msemaji wa kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu mjini Geneva alitoa mwito wa kuachiliwa bila masharti yoyote watu hao. Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linaendesha shughuli zake nyingi nchini Iraq kupitia shirika hilo la hilali nyekundu.

Wafanyikazi sita wa shirika hilo wamechiliwa huru na watekaji nyara hao lakini hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu mateka wengine waliobakia.