1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Wanajeshi wengine zaidi wa Marekani wauwawa nchini Iraq.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz2

Jeshi la Marekani limesema kuwa, waasi wamewauwa wanajeshi watano wa Marekani nchini Iraq.

Wanamaji wanne wa Marekani na baharia mmoja waliuwawa hapo jana kufuatia mapigano katika jimbo la Anbar.

Kufuatia vifo vya wanajeshi hao, idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa mnamo mwezi huu huko Iraq imefikia 96.

Shirika la habari la Ufaransa AFP limeripoti kuwa, karibu wanajeshi elfu tatu wa Marekani wameuliwa kwa mashambulio na wengine kwa ajali tangu Marekani ilipoivamia Iraq mwezi March mwaka 2003.

Wakati huo huo watu wenye silaha wameushambulia msafara wa magari ya polisi wa Iraq kaskazini mwa Baghdad na kuwauwa polisi wanane akiwemo Kamanda mmoja.

Kiasi cha polisi wengine 50 wameripotiwa kupotea muda mfupi tu baada ya shambulio la karibu na Bakuba.