1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:washia wapatana ?

7 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hm

Habari kutoka Irak zinasema kuwa viongozi wawili muhimu sana wa kishia wametiliana saini mapatano ya kuzuia mauaji.

Viongozi hao Moqtada al Sadr na Abdul Azizi al Hakim wamekuwa wanapambana vikali katika kuwania udhibiti wa sehemu zinazokaliwa hasa na washia .

Mapambano baina ya jamii tofauti nchini Irak zimekwamisha juhudi za waziri mkuu wa nchi hiyo bwana al Maliki zenye lengo la kuleta mageuzi yanayotakiwa na Marekani.