1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:watu 22 wameuwawa kufuatia mashambulio mawili ya mabomu

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7H4

Watu 22 wameuwawa kufuatia mashambulio mawili ya mabomu ya kutegwa ndani ya gari kaskazini mwa mji mkuu wa Baghdad nchini Irak.

Habari zaidi kutoka mjini Baghdad zinafahamisha juu ya kuuwawa wanawake wawili wakati mawakala wa usalama wa kampuni moja ya Australia walipowafyatulia risasi.

Kampuni hiyo ya usalama imekiri kuhusika na tukio hilo na tayari imeelezea masikitiko yake kwa serikali ya Irak.

Kampuni hiyo ya usalama imeahidi kuanzisha uchunguzi na wakati huo huo imesema itazilipa fidia familia za wanawake hao walio uwawa.

Mwezi uliopita watu 17 waliuwawa wakati mawakala wa usalama wa kampuni ya Kimarekani walipowafyatulia risasi.