1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Yadaiwa Moqtada al Sadr ametoroka Irak na kuingia Iran

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCS7

Jeshi la Marekani nchini Irak limesema kuwa lina sababu za kutosha kuamini kuwa kiongozi mwenye msimamo mkali wa madhehebu ya Shia Moqtada al Sadr ameondoka nchini Irak na kuingia nchini Iran.

Wafuasi wa Al Sadr wamesema kuwa kiongozi huyo bado yuko nchini Irak.

Jeshi la Marekani nchini Irak limesema lina amini kuwa kiongozi huyo ameondoka nchini humo, kutoroka msako mkubwa unaofanywa dhidi ya wanamgambo baada ya serikali ya Irak kufunga mipaka kati yake na Syria na Iran.

Washington imekitaja kikosi cha Mehdi kinacho ongozwa na Moqtada al Sadr kuwa ndio kikwazo kikubwa cha usalama wa Irak.