1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAIDOA: Somalia yaomba msaada wa dharura kuzuia janga la kiutu

19 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrH

Serikali ya Somalia hii leo imeomba msaada wa dharura kwa jumuiya ya kimataifa ili kuzuia janga la kiutu kutokana na mafuriko yaliotokea katika nchi hiyo kwenye Pembe ya Afrika.Waziri mkuu Ali Mohamed Gedi,ametoa mwito huo wakati idadi ya watu waliopoteza maisha yao katika mafuriko ya majuma matatu,imefikia kama 52 na zaidi ya 50,000 wamepoteza makazi yao.Si chini ya watu milioni 1.5 wameathirika na vile vile sehemu kubwa za mashamba zimeteketezwa kwa mafuriko.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,mafuriko hayo huenda yakawa mabaya kabisa kupata kushuhudiwa Somalia,tangu miaka 50 ya nyuma.