1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bajeti ya Rais Obama yapendekeza punguzo la matumizi ya serikali

Thelma Mwadzaya27 Februari 2009

Barack Obama, jana Alhamis amewasilisha mswada wake wa kwanza wa bajeti bungeni . Rais huyo mpya wa Marekani anapanga punguzo kubwa la matumizi ya serikali pamoja na ongezeko la kodi

https://p.dw.com/p/H2S8
Bajeti ya Rais ObamaPicha: picture-alliance/ dpa

Rais Barack Obama katika mswada wake wa kwanza wa bajeti amefika mbali. Tayari hivi sasa imepanda nakisi ya bajeti kwa mwaka ujao kwa kiasi cha dola bilioni 1,100. Kwa hiyo kiasi cha robo ya matumizi ya serikali yatagharimiwa kwa mikopo. Hii ni muhimu, amesema Obama ili kuweza kutoa msukumo kwa uchumi wa nchi hiyo na nchi hiyo kuweza kujitoa katika matatizo ya kiuchumi. Lakini kwa kipindi cha muda mrefu njia hiyo haifai kuendelea kutumiwa.''Ni kwa kuweka nidhamu ya matumizi ndipo tunaweza kuleta hali ya ukuaji wa uchumi na kuhakikisha kuleta ufanisi. Na hii ndio hasa nia ya bajeti hii ambayo naiwasilisha katika baraza la Congress leo.''


Hadi mwaka 2013, lakini , ameahidi rais Obama kuwa nakisi hiyo itakuwa imepunguzwa kwa nusu.

Obama ametumia bajeti hiyo mpya kujitenga na utawala wa mtangulizi wake George Bush. Tumerithi nakisi kubwa kabisa, yamesikika matamshi yake katika hotuba yake hiyo ya bajeti. Huu ni ushahidi wa kushindwa kwa utaratibu wa matumizi pamoja na sera za matumizi. Pekee katika mwaka huu wa bajeti nakisi ni kiasi cha dola bilioni 1.75.

''Nina nia ya kuleta mabadiliko ambayo watu waliyapigia kura Novemba mwaka jana . Na hii ina maana ya kupunguza kile tusichokihitaji na kulipia kile tunachokihitaji.''


Tayari hali imekuwa ya matatizo kuliko ilivyokuwa inaonekana mwanzoni. Kutokana na sheria na mikataba mbali mbali ya muda mrefu , robo tatu ya bajezi hii ya Marekani imekamilika. Ni kiasi cha robo tu ambayo bado inahitaji hatua za kuchukuliwa ili kuondoa matatizo.

''Leo hii tunahitaji kulenga katika misingi. Kwa kuwa tumerithi nakisi ya dola trilioni moja, na itatuchukua muda mrefu kuziba pengo hili. Tunahitaji kulenga katika kile ambacho tunakihitaji ili kusukuma uchumi wetu mbele na sio uzuri wa kile ambacho tunakipendelea.''


Hapa rais Obama anaweka wazi masuala muhimu na kuanza kutekeleza ahadi za uchaguzi. Kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mfuko kwa ajili ya huduma za afya, angependa katika muda wa miaka kumi ijayo Wamarekani wote wawe na bima ya afya, kwa kuwa kuna Wamarekani hivi sasa wapatao milioni 48 ambao hawana bima ya afya. Pamoja na hayo anataka kuwekeza pia katika elimu na nishati endelevu. Kwa hiyo ni muhimu kupunguza kodi kuanzia mwezi Aprili kwa Wamarekani wote wenye kipato chini ya dola 200,000 kwa mwaka.


ZR