1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAMAKO:Wafadhili kuahidi msaada mkubwa kwasababu ya homa ya ndege

7 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClj

Kiongozi anayesimamia athari za ugonjwa wa homa ya ndege katika Umoja wa Mataifa anatoa wito kwa wafadhili kuahidi takriban dola nusu bilioni kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kupambana na aina moja hatari ya virusi vya H5N1 vilevile kujilinda endapo virusi hivyo vitabadilika umbo na kusambaa kwa wanadamu.

Kulingana na kiongozi huyo David Nabarro,usambaaji wa virusi hivyo vya H5N1 katika ndege ulimwenguni umepungua kasi katika kipindi cha miezi michache iliyopita japo huenda vikazuka tena mapema mwaka ujao wakati ndege wanapoyakimbia maeneo ya baridi.

Anaongeza kuwa hatua zimepigwa katika kuimarisha uwekezaji wa sekta ya ufugaji wanyama japo bado kuna haja ya kuwa chonjo zaidi ili kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo endapo unatokea.

Mkutano wa kimataifa unaojadilia homa ya ndege ulifunguliwa rasmi hapo jana mjini Bamako .Mkutano huo wa siku tatu ni wa nne kufanyika tangu mwisho wa mwaka uliopita.

Kikao hicho kinafanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza kwasababu ya hofu kwamba virusi vya homa ya ndege huenda vikakita barani humo.Mpaka sasa mataifa manane yameathiriwa huku visa vipya vikiripotiwa katika mataifa matatu kati yao ya Nigeria,Sudan na Misri.

Virusi vya H5N1 vya homa ya ndege vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 150 tangu mwaka 2003 hasa katika mataifa ya Indonesia na Vietnam.

Kiongozi anayesimamia athari za ugonjwa wa homa ya ndege katika Umoja wa Mataifa anatoa wito kwa wafadhili kuahidi takriban dola nusu bilioni kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kupambana na aina moja hatari ya virusi vya H5N1 vilevile kujilinda endapo virusi hivyo vitabadilika umbo na kusambaa kwa wanadamu. Kulingana na kiongozi huyo David Nabarro,usambaaji wa virusi hivyo vya H5N1 katika ndege ulimwenguni umepungua kasi katika kipindi cha miezi michache iliyopita japo huenda vikazuka tena mapema mwaka ujao wakati ndege wanapoyakimbia maeneo ya baridi.Anaongeza kuwa hatua zimepigwa katika kuimarisha uwekezaji wa sekta ya ufugaji wanyama japo bado kuna haja ya kuwa chonjo zaidi ili kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo endapo unatokea.

Mkutano wa kimataifa unaojadilia homa ya ndege ulifunguliwa rasmi hapo jana mjini Bamako .Mkutano huo wa siku tatu ni wa nne kufanyika tangu mwisho wa mwaka uliopita.Kikao hicho kinafanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza kwasababu ya hofu kwamba virusi vya homa ya ndege huenda vikakita barani humo.Mpaka sasa mataifa manane yameathiriwa huku visa vipya vikiripotiwa katika mataifa matatu kati yao ya Nigeria,Sudan na Misri.

Virusi vya H5N1 vya homa ya ndege vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 150 tangu mwaka 2003 hasa katika mataifa ya Indonesia na Vietnam.