1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban achaguliwa tena kuongoza umoja wa mataifa

Sekione Kitojo22 Juni 2011

Baraza kuu la umoja wa mataifa limemchagua tena Ban Ki-moon kuwa katibu mkuu wa taasisi hiyo kwa kipindi cha pili cha miaka mitano.

https://p.dw.com/p/11h3S
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon aliyechaguliwa upya jana .Picha: AP

Baraza kuu la umoja wa mataifa limemchagua Ban Ki-moon kuwa katibu mkuu wa taasisi hiyo ya kimataifa kwa kipindi cha pili cha miaka mitano. Ban amesema mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa kwake, akieleza mapambano dhidi ya ongezeko la ujoto duniani kuwa ni suala muhimu zaidi kwa binadamu. Kipindi chake cha pili cha miaka mitano kitaanza Januari mosi na kufikia mwisho mwaka 2016. Ban alitangaza kugombea wadhifa huo wiki mbili zilizopita na kupewa uungwaji mkono rasmi na baraza la usalama la umoja wa mataifa Ijumaa iliyopita. Akiwa hana mpizani kulazimisha mpambano , baraza kuu la umoja wa mataifa lenye wanachama 192 limeidhinisha kipindi hicho kipya kwa kauli moja.