1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki-Moon ahimiza suluhisho la Darfur

P.Martin5 Septemba 2007

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekwenda Juba,mji wa kusini mwa Sudan.

https://p.dw.com/p/CB1W

Lengo la ziara ya Katibu Mkuu Ban,ni kujaribu kuhimiza utekelezaji wa makubaliano ya amani ya yaliyotiwa saini mwaka 2005.

Hapo awali Ban alikutana na Rais Omar el-Bashir wa Sudan mjini Khartoum na alisema, walijadiliana njia za kuharakisha kupeleka Darfur vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Vile vile alimuarifu Rais el-Bashir juu ya juhudi zake na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika,kuhimiza majadiliano ya amani kuhusu Darfur pamoja na makubaliano kamili ya amani.