1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban kupitia upya sera ya MONUC.

Halima Nyanza7 Oktoba 2010

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anapitia upya sera na operesheni za kikosi cha kulinda amani cha umoja huo, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kufuatia mapigano na tukio la ubakaji wanawake zaidi ya 300.

https://p.dw.com/p/PXdR
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha: AP

Ban Ki Moon amesema Umoja wa mataifa unapaswa kuwa wenye uhalisi, na amekiri kuwepo kwa idadi ndogo ya walinda amani hao, ambao wameelemewa na ukubwa wa nchi hiyo, pamoja na udogo wa rasilimali zao.

Kongo Blauhelm-Soldaten
wanajeshi wa Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo -Monuc- wakipiga doria.Picha: picture-alliance/dpa

Kikosi hicho cha kulinda amani cha umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, mara kadhaa kimekuwa kikikosolewa kwa kutokuwa na uwezo wa kuzuia visa vya ubakaji, matukio ambayo yalitokea kwa siku kadhaa julai mwaka huu na eneo ambalo liko kilomita 20 kutoka katika makao ya kikosi hicho.

Flash-Galerie UN Millennium Ziele 6 Krankheiten bekämpfen
Wanawake na watoto, wako katika hatari zaidi ya kubakwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,.Picha: AP

Wiki hii, Umoja wa Mataifa umethibitisha kwamba  kiongozi wa waasi wa MaiMai Cheka, kundi ambalo linadaiwa kufanya uhalifu huo wa ubakaji, Luteni kanali Mayele amekamatwa.