1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGLADESH:Mamilioni waathirika na mafuriko Asia

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcH

Pepo kali za msimu katika bahari ya hindi zimesababisha mafuriko katika maeneo ya kusini mwa Bara la Asia ambapo zaidi ya watu millioni 20 wameathirika.

Tishio la kulipuka mwa maradhi yanayosababishwa na mafuriko limezidi kuongezeka huku vijiji kadhaa vimekiwa vimefunikwa na maji.

Inaarifiwa ya kwamba zaidi ya nusu ya eneo la Bangladesh imefunikwa na maji, ambapo eneo la kaskazini mwa India na Nepali hali ni kama hiyo.

Mashirika ya kimataifa ya misaada yametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa misaada.

Zaidi ya watu 1000 Kusini mwa Asia wamekufa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa toka zilipoanza kunyesha katikatika ya mwezi wa sita.

Wakati huo huo Rais George Bush wa Marekani ametangaza kuwa nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa mwishoni mwa mwezi ujayo.

Waziri wa Mambo ya Nje Condoleza Rice anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa mkutano huo utakaojaribu kuangalia njia za kuchukua kuzuia uchafuzi wa hali ya hewa.

Hali mbaya ya hewa iliyoikumba Ulaya hivi karibuni imeelezwa inatokana na kuongezeka kwa ujoto wa dunia ambao unachangiwa na uchafuzi wa hewa .