1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bara la Afrika kupewa Dollar Billioni 60

Omar Mutasa8 Juni 2007

Viongozi wa Mataifa tajiri kiviwanda wanaohudhuria mkutano wa G8 katika mji wa Heilligendamm hapa Ujerumani, wameahidi kutoa Dollar Billioni 60, ili kupambana na maradhi ya Ukimwi , Malaria na Kifua kiku katika Bara la Afrika.

https://p.dw.com/p/CHCz
Rais wa Ghana na Kansala Angela Markel wa Ujerumani
Rais wa Ghana na Kansala Angela Markel wa UjerumaniPicha: AP

Akitangaza habari hizo waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Bi Heidemarie Wieczorek-Zeul,

amesema kati ya $ Billioni 60, sawa na Euro na Billioni 44.8 , Serekali ya US itatoa nusu ya kiwango hicho na Ujerumani kutoa Euro Billioni 4.

Rais BUSH ambae tayari alianzisha mradi wa kupambana na Ukimwi mwezi May huenda asiweko kwenye kikao cha leo kutokana na kuumwa tumbo, lakini Afisa wa White House amesema hali ya Rais Bush sio mbaya kiasi hicho. Jana Rais Bush hakuweza kuzungumza na waandishi wa Habari.

Nae Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy bada ya kuzungumza na Rais Bush ,amesema, Rais Bush amekua hajisikii vizuri Asubuhi ya leo lakini huenda akaungana nao wakati wowote

Siku ya leo.
Mkutano huu wa G8 umewaleta pia Marais Thambo Mbeki wa Afrika Kusini na Rais Hu Jintao wa Uchina mazungumzo yao na viongozi hao wa kundi la G8 yakitarajiwa kuzungumzia misaada zaidi kwa Nchi zinazoinukia.

Pembeni mwa mkutano huo wa kilele wa Heillegendamm, Rais John Koffour wa Ghana

amekueko na amesema ;Afrika inalitegemea kundi la nchi 8 kutimiza ahadi inazotoa ,na kwa upande wa Afrika tunaahidi kutimiza tulichoahidi,ili kwamba huu uwe ushirikiano wa kweli.

Pia tuanzishe chombo cha kuona kwamba pande zote zinawajibika,kuhakikisha kwamba pande zote zinatimiza ahadi.

Viongozi wa kundi hilo la G8 wamekutana na viongozi wa nchi za Afrika kutoka Misri,

Algeria ,Senegal, Ghana na Nigeria na ilikubaliwa kuongeza misaada ya maendeleo na pia kufanyike marekebisho.

Kuhusu matokeo jumla ya mkutano wa kilele wa Heillegendamm, hasa kuhusu suala la ulinzi wa Mazingira ,mwenyekiti wa mkutano huo Kansala Angela Markel wa Ujerumani alisema, Kutokana na suluhisho lililofikiwa ,

naweza kuishi nalo kwa uzuri, nahisi hayo ni maendeleo makubwa na matokeo mazuri. Kwanza tumefanikiwa kwamba nchi zote nane zimetambua matokeo yatakayofuata kutokana na taarifa juu ya hali ya hewa duniani,na pia ile ripoti ya IPCC.

La pili na kwamba tumekubaliana tuwe na lengo la kima cha kupunguza moshi mchafu hewani ,na lengo hilo liwe la lazima. Pia kumetajwa kwamba kile ambacho Japan,Kanada na hasa nchi za Umoja wa ulaya, zimependekezwa kitiliwe maanani. kwamba angalau hadi mwaka 2050 lazima moshi mchafu unaoingia hewani upunguzwe kwa nusu . Kwangu mimi hilo ni muhimu sana na yote hayo yafanyike chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa.

Mshauri wa shirika la kupambana na mazingira la Green peace, Daniel Mittler,

amesema hayo yaliokubaliwa hayatoshi kubadilisha au kupunguza hali ya ujoto duniani

Lakini afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, ameyakaribisha mapatano hayo yaliofikiwa, na kwamba kumepatikana ridha ya kupunguza moshi wa viwandani hadi ifikapo mwaka 2050, kwa maneno mengine kupindukia muda uliowekwa wa mkataba wa Kyoto Japan wa mwaka 2012.