1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barack Obama amshinda John McCain kuwa rais wa 44 wa Marekani.

5 Novemba 2008
https://p.dw.com/p/Fneb
Barack Obama akiwa na mkewe Michelle wakati wa moja wapo ya kampeni za uchaguzi.Picha: AP

Mgombea Urais wa chama cha Democrats nchini Marekani amemshinda mpinzani wake John McCain kutoka chama cha Republican kuwa rais wa 44 wa Marekani. Obama aliendesha kampeni kabambe kwa muda wa miaka miwili kwanza akishinda nafasi ya kuwa mgombea kawa niaba ya chama chake alipochuana vikali na Hillary Clinton na baadae kushinda uchaguzi wa Rais wa taifa hilo kubwa duniani. Mpigania maarufu wa haki za kiraia Jesse Jackson alionekana akitokwa na machozi. John McCain alihutubia wafuasi wake akiwashukuru na kumpongeza Obama ambaye alisema ameshazungumza naye kwa simu. Pia Rais George W.Bush alimpigaia simu Obama kumpongeza. Obama mwenye umri wa miaka 47,mwanasiasa aliyechanganya damu akitokana na Baba mwafrika kutoka Kenya na Mama mzungu kutoka Hawai atakua Mmarekani wa kwanza mweusi kuchaguliwa Rais katika historia ya nchi hiyo.