1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mswada wa bajeti

Abdu Said Mtullya16 Desemba 2009

Mawaziri wa Ujerumani waupitisha mswada wa bajeti.

https://p.dw.com/p/L3vD
Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble akifafanua mswada wa bajeti kwa waandishi habari.Picha: AP

Baraza la mawaziri la Ujerumani leo limeyapitisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka ujao wa fedha.

Lakini mapendekezo hayo yamelaumiwa vikali na vyama vya upinzani kwa sababu yataiwezesha serikali kuongeza deni.

Mswada wa bajeti uliowasilishwa na waziri wa fedha Wolfgang Schäuble unatoa mwanya kwa serikali wa kuongeza deni kwa Euro bilioni 85.8 Huo ni mswada wa kwanza wa bajeti kupitishwa tokea kuundwa serikali mpya ya vyama vya kihafidhina CDU,CSU na chama cha waliberali FDP kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi septemba mwaka jana.Kiwango hicho cha deni hakijawahi kufikiwa katika historia ya hivi karibuni nchini Ujerumani

Kwa mujibu wa mapendekezo yaliyowasilishwa na waziri wa fedha mfuko wa matumizi pia unatarajiwa kuongezeka hadi Euro bilioni 325.4 hasa kutokana na mipango ya kukabiliana na athari za mgogoro wa uchumi.

Waziri wa fedha bwana Schäuble ametetea mapendekezo hayo. Amesema japo ni kama shubiri, ni sahihi, kiuchumi na kisiasa.

Lakini mswada huo umekosolewa vikali na vyama vya upinzani.Mwenyekiti wa chama cha kijani Claudia Roth amesema mswada huo unaonyesha mipango muflisi ya serikali.Bibi Roth ameilaumu serikali hasa kwa sababu zaidi ya theluthi moja ya mfuko wa matumizi itatokana na kuongeza deni.

Mwandishi/Mtullya/DPA/ZA.

Mhariri/Abdul-Rahman