1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barghouti kuachiwa na Israel ?

5 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/CklF

AMMAN:

Rais wa mamlaka ya Ndani wa Palestina Mahmud Abbas ameondoka Jordan kuelekea Riyadh,Saudi Arabia kushauriana na mfalme Abdullah juu ya hali ya mazungumzo ya amani ya Mashariki ya kati kabla rais George Bush hakuwasili huko wiki hii ijayo-duru za wapalestina zimearifu.

Rais Bush anaetarajiwa kuzuru Israel na ardhi za wapalestina amepinga mpango wa Israel wa kutanua ujenzi wa maskani za wayahudi katika ardhi za wapalestina.

Taarifa kutoka Jeruselem zasema,makamo waziri wa ulinzi wa Israel,Matan Vilnai alisema leo kwamba angekuwa tayari kumtoa gerezani mfungwa mashuhuri wa kipalestina ili kumkomboa mwanajeshi wa Israel alienyakuliwa na chama cha Hamas hapo juni, 2006.Marwan Barghouti,anaangaliwa kuwa ni mtu barabara kumrithi rais wa sasa wa Mamlaka ya ndani was Palestina Mahmud Abbas.