1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BASRA: Wanajeshi wa Uingereza washambulia kituo cha polisi, Iraq

26 Desemba 2006

Kiasi cha wanajeshi 1000 wa Uingereza wamevamia kituo kimoja cha polisi katika mji wa Basra na kuwaua wapiganaji saba. Hatua hiyo ilichukuliwa kuwazuia askari polisi kuwaua wafungwa. Wanajeshi wa Uingereza walilipua jengo husika mara baada ya kuwahamisha wafungwa hao walioonyesha dalili kwamba walikuwa wameteswa. Mahabusu zaidi ya 120 waliokolewa. Kwengineko, mjini Baghdad, mashambulizi mawili ya mabomu yalitokea ambapo bomu lililotegwa ndani ya gari lilipuka karibu na soko huku mlipuaji wa kujitoa mhanga akijilipua ndani ya basi. Mashambulizi hayo yalisababisha mauaji ya watu 14 na wengine 33 wakajeruhiwa.

https://p.dw.com/p/CBHo