1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern, Dortmund zatinga awamu ya mchujo

7 Novemba 2014

Bayern Munich imefuzu kwa urahisi katika awamu ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa kuizaba AS Roma magoli mawili kwa sifuri. Lakini mambo yalikuwa magumu kwa Schalke nchini Ureno

https://p.dw.com/p/1DipV
Champions League FC Bayern München AS Rom 5.11.2014
Picha: picture-alliance/dpa/Tobias Hase

Hawakufunga magoli saba mara hii, lakini Bayern ndiyo klabu ya kwanza ya Ujerumani kuenya moja kwa moja katika awamu ya mchujo huku zikiwa zimesalia mechi mbili za kuchezwa katika awamu ya makundi.

Bayern imeweka rekodi ya asilimia 100 katika awamu ya makundi baada ya kucheza mechi nne. Manchester City walibamizwa na CSKA Moscow katika mchuano mwingine wa kundi hilo. Moscow waliiduwaza City kwa kuifunga magoli mawili kwa moja mjini Manchester.

Mjini Lisbon hata hivyo, vijana wa Rpberto Di Matteo, Schalke walisakamwa na Sporting Lisbon kwa kufungwa magoli manne kwa mawili.

Champions League Sporting Lissabon FC Schalke 05.11.2014
Vijana wa Roberto Di Matteo walikuwa na usiku mrefu mjini LisbonPicha: Alex Grimm/Bongarts/Getty Images

Dortmund yapenya

Dortmund iliishinda tena Galatasaray kwa kuifunga mabao manne kwa moja na kujikatia tikiti ya awamu ya mchujo. Vijana hao wa Jurgen Klopp wamekuwa na mwanzo mbaya kabisa katika ligi ya nyumbani Budnesliga, lakini wanaonekana kupepea katika jukwaa la Ulaya. Bayer Leverkusen iliishinda Zenit St Petersburg mabao mawili kwa moja katika mchuano wa ugenini.

Kwingineko Ulaya.

Licha ya magoli mawili kutoka kwake Alexis Sanchez, Arsenal waliduwazwa kwa kutoka sare ya magoli matatu kwa matatu dhidi ya Anderlecht katika uwanja wao wa nyumbani. Hiyo ni licha ya kuwa Arsenal walikuwa kifdua mbele magoli matatu kwa sifuri kabla ya Anderlecht kujituma na kuushangaza umati wa Emirates. Karim Benzema alifunga goli pekee lililoipa ushindi Real Madrid dhidi ya Liverpool wakati Basel ikiwararua Ludogorots mabao manne kwa sifuri katika mechi nyingine ya kundi B.

Juventus imeyumbayumba barani Ulaya msimu huu, lakini ilipata ushindi wa nyumbani wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Olympiakos. Benfica iliishinda Monaco goli moja kwa sifuri wakati Atletico Madrid ikipata ushindi mgumu wa mabao mawili kwa bila ugenini dhidi ya Malmo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Rueters
Mhariri: Sekione Kitojo