1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kuvaana na Benfica robo fainali

18 Machi 2016

Droo ya ratiba ya hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya imewekwa hadharani ambapo machampioni watetezi wa ligi kuu ya kandanda nchini Ujerumani Bayern Munich wataanza hatua hiyo wakivaana na Benfica

https://p.dw.com/p/1IG6f
Baadhi ya wachezaji wa Bayern Munich ya nchini Ujerumani.
Baadhi ya wachezaji wa kilabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.Picha: picture-alliance/dpa/P. Kneffel

Wolfsburg ya Ujerumani itachuana na miamba ya Uhispania Real Madrid. Wolfsburg haijawahi kushinda kombe hilo la Ulaya.

Mabingwa watetezi Barcelona wamepewa klabu nyingine ya Uhispania, Atlético Madrid mechi hiyo ikiwa kama marudio ya robofainali msimu wa 2013/14. Atlético walishinda 1-0 na mechi ya ugenini ikaisha sare ya 1-1. Klabu ya Manchester City imepewa miamba wa Ufaransa Paris Saint Germain ambao tayari wameshinda ligi ya kandanda nchini humo huku kukisalia mechi nane msimu kukamilika

Mechi hizo za robofainali zitachezwa 5/6 na 12/13 Aprili

Katika droo ya dimba la UEFA Europa League

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp atakutana na timu yake ya zamani Borussia Dortmund ya Ujerumani. Klopp mwenye umri wa miaka 48 aligura BVB msimu uliopita baada ya kuiongoza kutwaa mataji mawili ya Bundesliga na kufika katika fainali ya vilabu bingwa Ulaya.

Sevilla, ambayo italenga kunyakua kombe hilo kwa mara ya tatu na itakwaruzana na Athletic Bilbao. Villareal itachuana na timu ya Czech Sparta Prague huku kilabu ya Ureno Braga ikikabiliana na Shakhtar Donetsk kutoka Ukraine. Mechi hizo za robo fainali zitachezwa mnamo tarehe 7 na 14 mwezi Aprili

Mwandishi: Isaac Gamba
Mhariri: Mohamed Abdul- Rahman