1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich yashindwa kumaliza kazi ya ubingwa

Sekione Kitojo
13 Mei 2019

Bayern Munich yaweka uamuzi wa  ubingwa  wa  Ujerumani  rehani, hadi  mchezo wa  34  Jumamosi  ijayo.

https://p.dw.com/p/3IQy2
Fußball Bundesliga RB Leipzig v Bayern München Spielszene
Pambano kati ya Bayern na RB LeipzigPicha: Getty Images/AFP/O. Andersen

Mvutano  kama  uliotokea  katika  Premier League  unaonekana kujitokeza  pia  katika  Bundesliga msimu  huu. Bayern  Munich inaongoza msimamo  wa  ligi  kwa  kuwa  na  pointi 75 , wakati hasimu  wake  wa  karibu  Borussia  Dortmund  ina  pointi 73.

Fußball Bundesliga RB Leipzig v Bayern München  Fans
Mashabiki wa bayern wakiipa moyo timu yao ilipopambana na RB Leizig , na kutoka sare bila kufunganaPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Ni mchezo  wa  mwisho  wa  34  utakaoamua  nani  anabeba  ngao  ya ubingwa  katika  Bundesliga  msimu  huu. Iwapo Bayern itaondoka na  ushindi, ikihitaji  sare  tu kunyakua  ngao  hiyo  kwa  mara  ya saba  mfululizo, hilo  ni  suala  la  kusubiri  na  kuona. Bayern Munich itakuwa  nyumbani  katika  mchezo  wake  huo ikiwakaribisha Eintracht  Frankfurt, wakati  Borussia  Dortmund  itakuwa  ugenini ikipambana  na  Borussia  Moenchengladbach.

Bayern Ilishindwa mwishoni  mwa  juma  kukamilisha  ubingwa  wake  wa  saba  baada ya  kutoka  sare  ya  bila  kufungana  na  RB Leipzig katika  uwanja wa  Red Bull  Arena  siku  ya  Jumamosi.

Fußball: 1. Bundesliga, Borussia Dortmund - Fortuna Düsseldorf
Borussia Dortmund ina matumaini kwamba Bayern Munich itateleza katika mchezo wa mwisho wa ligi msimu wa mwaka 2018/19Picha: Reuters/L. Kuegeler

Hata  hivyo  wachambuzi  wanaona  hakutakuwa  na  kazi  kubwa kwa  Bayern  kukamilisha  ubingwa  wake  wa  saba  mfululizo itakapokumbana  na  Frankfurt  ambayo  baada  ya  kutolewa  katika mchezo  wa  nusu  fainali  ya  Europa League  kwa  mikwaju ya penalti  dhidi  ya  Chelsea  ya  Uingereza, nguvu  zimewaishia  na hawatakuwa  na  ubavu  wa  kuizuwia  Bayern kunyakua  taji  lake hilo  la  saba. Lakini  mpira  unadunda  na  kila  kitu  kinawezekana. Na  hapo  ndio matumaini  ya  Borussia  Dortmund  yanapojikita.

Frankfurt  ilitandikwa  mabao 2-0  jana  jumapili  na  Mainz 05 katika mchezo  wa  mwisho  wa  kukamilisha  duru  ya  33  ya  Bundesliga.