1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING : China kuchambuwa upya hukumu za kifo

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCxE

China imetangaza mipango ya kuzichambuwa upya maelfu kwa maelfu ya hukumu za kifo kuanzia mwezi wa Januari ili kuzuwiya watuhumiwa kuhukumiwa kwa makosa.

Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu Amnesty International limesema China imewanyonga takriban watu 1,770 hapo mwaka jana.Uamuzi huo unavuwa madaraka yaliyokasimiwa mahkama za majimbo hapo mwaka 1983.Jaji Mkuu Xiao Yang amesema uchambuzi wa hukumu hizo za kifo utakaofanywa na Mahkama Kuu ya Wananchi wa China utawapa watuhumiwa nafasi moja zaidi ya kujitetea.

Katika miaka ya hivi karibuni vyombo vya habari vya China vimefichuwa ukiukaji kadhaa wa sheria unaofanywa na mahkama za majimbo.