1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Kikao cha baraza la taifa waanza.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCM4

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao ameitaka nchi yake kupambana na kile alichokisema kuwa ni ukuaji usiokuwa imara wa kiuchumi pamoja na matumizi yaliyopita kiasi ya nishati.

Ametoa matamshi hayo wakati akifungua kikao cha kila mwaka cha baraza la taifa la Congress, ambalo ni kama bunge la chama tawala cha Kikomunist.

Amekwenda umbali wa kuahidi kuchukua hatua kuhifadhi nishita, kulinda mazingira na kupambana na tofauti ya hali ya maisha. Viongozi wa Kikomunist wanajaribu kuimarisha matumizi mazuri ya nishati nchini humo pamoja na utegemezi wa mafuta kutoka nje, hali ambayo wanaiona kuwa ni udhaifu kimbinu. Kabla ya mkutano huo China ilitangaza ongezeko la matumizi ya kijeshi kwa mwaka 2007 kwa zaidi ya asilimia 18.