1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Mafuriko yaendelea nchini China

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgJ

Nchini China zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha yao katika mafuriko na mmomonyoko wa ardhi.Shirika la habari la China Xinhua limeripoti habari hiyo na kueleza kuwa watu 59 walikufa katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua na vimbunga katika Wilaya ya Yunnan.Wengine wasiopungua 40 hali kadhalika walipoteza maisha yao katika dhoruba,kwenye wilaya ya pwani ya Shandong,mashariki mwa nchi.Tangu majira ya joto kuanza mwaka huu,mamia ya watu wamekufa katika mafuriko makubwa yaliyoikumba takriban nusu ya China.Kina cha maji ukingoni mwa mto Huai mashariki ya China kinatazamiwa kubakia juu na hali hiyo ya hatari huenda ikaendelea kwa siku kumi zijazo.Maelfu ya watu wamelazimika kuondoka makwao.