1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Mazungumzo yasitishwa.

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBLG

Mazungumzo ya nchi sita yenye lengo la kusitisha mpango wa kinuklia wa Korea ya kaskazini yamesitishwa kwa muda wa siku mbili wakati washiriki wakichunguza maelezo ya muswada juu ya kuvifunga vinu vya kinuklia.

Mjumbe maalum wa China katika mazungumzo hayo amesema kuwa maelezo juu ya waraka huo hayatatolewa hadi pale serikali za Korea ya kaskazini, China, Japan , Russia, Marekani na Korea ya kusini zitakapopata muda wa kuyatathmini.

Wajumbe wa majadiliano mjini Beijing wamekuwa wakijaribu kusukuma mbele makubaliano ya mwezi February ambapo mataifa hayo yalikubaliana kuipatia Korea ya kaskazini tani milioni moja za mafuta mazito, ama thamani sawa ya fedha katika misaada mingine. Kwa upande wake Korea ya kaskazini ilikubali kufunga kinu chake kikuu na kuachana kabisa na mipango yake yote ya kinuklia.