1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Merkel aendelea na ziara yake China

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVS

Kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel, leo ameishawishi China iheshimu sheria za kimatiafa za kibiashara na maendeleo.

Bi Merkel ameyasema hayo katika mkutano wake wa kwanza rasmi na waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, juu ya njia za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na China.

Aidha kansela Merkel amesema ingawa kila nchi ina haki ya kijiendeleza kiuchumi, ipo haja ya kuheshimu sheria za kibiashara za kimatiafa.

Bi Merkel alizungumzia haki miliki na ubora wa bidhaa, maswala ambayo China inalaumiwa kwa kutoyazingatia.

Kansela Merkel amesema inawezekana kuendelea vizuri kiuchumi kwa pamoja katika ulimwengu unaoendelea kukua, iwapo sheria zitaheshimiwa.

Waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, kwa upande wake ameihakikishia Ujerumani na mataifa mengine kwamba kuendelea kukua kwa kasi kubwa uchumi wa China si tishio kwa ulimwengu na kuahidi kuwa nchi hiyo itashirikiana na nchi nyengine duniani pasipo vitisho.