1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Mkutano wa kilele wa viongozi wa Kiafrika na China

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwJ

Viongozi kutoka zaidi ya nchi 40 za Kiafrika wamekusanyika Beijing kwa mkutano wa kilele pamoja na China.Uhusiano wa kibiashara na vitega uchumi ni masuala yatakayotawala mkutano huo. China inatazamiwa kutangaza mipango ya misaada, biashara na maendeleo ya kijamii kwa nchi za Kiafrika.Msemaji wa wizara ya kigeni ya China,Liu Jiancho amekataa kutaja tarakimu kuhusika na misaada na mikopo hiyo.Vile vile alipuuza shutuma za wakosoaji kuwa China inatenda aina ya ukoloni mambo leo.Mwaka huu,biashara ya China pamoja na nchi za Kiafrika inatazamiwa kupindukia Dola bilioni 50.