1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Negroponte ziarani nchini China

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMl

Makamu wa waziri wa nje wa Marekani,John Negroponte amewasili Beijing nchini China,akiwa katika ziara ya kutembelea madola matatu,barani Asia.Hii ni ziara yake ya kwanza katika nchi za ngámbo tangu kushika wadhifa wake hivi karibuni. Baada ya kuwasili kutoka Tokyo,Negroponte alikutana na viongozi wa China,ikisemekana kuwa mada kuu katika majadiliano yao ni mradi wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini.Alipokuwa Japan, Negroponte alisema,serikali ya Pyongyang inapaswa kuchukua hatua muhimu kusitisha mradi wake wa nyuklia,kabla ya Marekani kufikiria kuondosha vikwazo.Negroponte anakamilisha ziara yake barani Asia kwa kuitembelea Korea ya Kusini.