1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Rais wa Ujerumani ziarani China

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByY

Rais Horst Köhler wa Ujerumani akiwa ziarani nchini China,amekutana na Waziri Mkuu Wen Jiabao.Viongozi hao wamesifu uhusiano mzuri wa kiuchumi uliopo kati ya nchi zao.Ujerumani pia inanufaika kutokana na uchumi wa China unaokuwa kwa kasi.Siku ya Alkhamisi,Köhler alikutana na Rais Hu Jintao na alitoa mwito wa kufanywa majadiliano pamoja na China juu ya masuala yenye utata.Kibiashara barani Ulaya,Ujerumani ni mshirika muhimu kabisa wa China.