1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Wafanyikazi wa China waachiwa huru Nigeria

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCV3

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya China imetangaza wafanyikazi tisa wa nchi hiyo waliotekwa nyara mwezi uliopita nchini Nigeria wameachiwa huru.

Wafanyikazi hao walitekwa nyara na watu waliokuwa na bunduki tarehe ishirini na tano mwezi uliopita katika jimbo la Bayelsa kutoka kwenye afisi za Kampuni ya Taifa ya China ya mafuta ya Petroli.

Wafanyikazi wa kigeni hasa kwenye sekta ya mafuta, wamekuwa wakilengwa sana na wanamgambo wenye bunduki wanaotaka nyongeza ya faida inayotokana na biashara ya mafuta.

Watu hao wameachiwa huru wakati ambapo Rais wa China, Hu Jintao, anaendelea na ziara yake ya mataifa manane barani Afrika kwa nia ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara.