1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing.Korea ya kaskazini kupatiwa fedha zake zilizozuiliwa.

20 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHK

Mazungumzo ya nchi sita kuhusiana na azma ya Korea ya kaskazini ya kujipatia silaha za kinuklia yataendelea mjini Beijing leo.

Katikati ya mwezi Februari, Korea ya kaskazini ilikubali kufunga kinu chake kikuu cha kinuklia katika muda wa siku 60 ili kuweza kupatiwa misaada ya fedha.

Wanadiplomasia wamesema jana kuwa makubaliano yamefikiwa kuachia baadhi ya fedha za Korea ya kaskazini zilizozuiliwa katika benki ya Macau, ikiondoa kikwazo kikubwa katika majadiliano hayo.

Marekani imekubali kuruhusu kuhamishwa kwa dola milioni 25 kutoka Banco Delta Asia nchini Macau kwenda katika akaunti ya Korea ya kaskazini nchini China.