1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Hezbollah yataka uchaguzi wa mapema

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiF

Upinzani nchini Libnan, unaoongozwa na kundi la Hezbollah linaloiunga mkono Syria, unataka uchaguzi wa mapema ufanyike katika juhudi za kuutanzua mgogoro wa kisiasa nchini Libnan. Haya yanafuatia hatua ya serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora kukataa kuundwa kwa serikali mpya ya umoja wa taifa.

Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakifanya maandamano makubwa tangu Disemba mosi wakitishia kuipindua serikali ambayo wanasema si halali tangu mawaziri sita wanaoiunga mkono Syria walipojiuzulu mwezi uliopita. Kiongozi wa jumuiya ya nchi za kiarabu, Amr Moussa, amekuwa akijaribu kuzipatisha pande hizo mbili, lakini hakuna ufanisi mkubwa uliopatikana mjini Beirut juma lililopita.