1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Majeshi ya Lebanon yanaendelea kupambana na wakimbizi wa Kipalestina.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzo

Vifaru vya jeshi la Lebanon vinaendelea kushambulia wanamgambo katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina kaskazini ya nchi hiyo kwa siku ya pili mfululizo.

Jeshi linapambana na wanamgambo wa Kipalestina ambao inadaiwa wanamahusiano na kundi la kigaidi la kimataifa la al-Qaeda pamoja na watu wenye imani kali nchini Syria.

Duru ndani ya kambi hiyo zinasema kuwa raia tisa wameuwawa leo katika mashambulizi hayo.

Kwa jumla kiasi watu 55 wameuwawa katika mapigano hayo.

Baraza la mawaziri la Lebanon linakishutumu kikundi cha Fatah al –Islam kwa kujaribu kuidhoofisha serikali katika wakati ambapo umoja wa mataifa unajaribu kuunda mahakama ya kimataifa itakayowahukumu watuhumiwa wa mauaji ya mwaka 2005 ya waziri mkuu Rafik Hariri.