1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Nasrallah aapa kuiangusha serikali ya Siniora.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClV

Kiongozi wa Hizboullah Sheikh Hassan Nasrallah ameapa kuwa yeye pamoja na wafuasi wake wataendelea na maandamano yao dhidi ya serikali ya Lebanon ya waziri mkuu Fouad Siniora. Lengo la mwisho kwa mujibu wa Nasrallah ni kuiangusha serikali hiyo inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.

Tangu Ijumaa iliyopita , maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana dhidi ya Siniora katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Wanaushutumu utawala wake kwa kushindwa kuiunga mkono Hizboullah wakati wa vita vya wiki sita dhidi ya Israel katikati ya mwaka huu.

Serikali ya Siniora inashaka kuwa Hizboullah inajaribu kuzuwia uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na mauaji ya waziri mkuu wa zamani Rafik Hariri, ambaye aliuwawa February 2005.