1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Pierre Gemayel azikwa kijijini kwake

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpw

Jeneza la waziri wa viwanda wa Lebanon aliyeuawa Pierre Gemayel, limefikishwa katika kijiji chake cha Asili cha Bikfaya kwa mazishi baada ya maelfu ya watu kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 34 katika kanisa la Wamaroniti la Saint George mjini Beirut.

Katika hotuba mbali mbali za wanasiasa wa karibu na nchi za magharibi akiwemo baba mzazi wa marehemu, rais wa zamani Amin Gemayel, wamesema Lebanon inahitaji mabadiliko ya viongozi na wametoa mwito wa kutolewa madarakani rais Emile Lahoud, anayoungwa mkono na Syria. Pierre Gemayel, mwanasiasa mkristu na mpinzani wa Syria, alipigwa risasi na kuuawa pamoja na mlinzi wake wakati akisafiri na gari lake mjini Beirut siku ya jumanne wiki hii.

Mashabiki wake wanaituhumu Syria kuhusika na mauaji hayo japokuwa Syria imekana kuhusika kwa njia yoyote yile.