1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Vikosi vimeingia kambi ya Nahr al-Bared

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiR

Vikosi vya Lebanon vimesonga mbele ndani ya kambi ya wakimbizi wa Kipalestina,kwa mara ya kwanza tangu mapambano kuzuka zaidi ya majuma manane yaliyopita.Bendera za Lebanon zimeonekana zikipepea ndani ya kambi ya Nahr al-Bared kwenye kama majengo mawili yaliyobomoka.Hatua hiyo inatoa sura mpya kwa mapambano kati ya wanajeshi wa Lebanon na wanamgambo wa Fatah al-Islam,kuwa vikosi havitoingia kambi za wakimbizi za Wapalestina nchini humo.Machafuko yanaendelea, huku wanasiasa wa Lebanon,ikiwa ni pamoja na wanachama wa kundi la madhehebu ya Kishia la Hezbollah,wakikutana karibu na mji mkuu wa Ufaransa,Paris.Viongozi hao wanatafuta njia za kumaliza mgogoro wa kisiasa kabla ya kufanywa uchaguzi wa rais Septemba ijayo.