1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Waziri mkuu akataa mawaziri kujiuzulu.

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtb

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora amekataa kukubali kujiuzulu kwa mawaziri watano wanaoiunga mkono Syria baada ya wiki ya mikutano kadha yenye lengo la kuwapa usemi zaidi katika serikali kuvunjika.

Mawaziri hao ambao walitoa barua zao za kujiuzulu ni wanachama wa muungano wa vyama vya Washia , Hizboullah na Amal.

Mazungumzo hayo yalivunjika kutokana na madai ya Hizbollah kuwa vyama vinavyoiunga mkono Syria vipewe nyadhifa za kutosha katika baraza la mawaziri ili kuwaruhusu kuzuwia maamuzi ya bunge.

Mazungumzo hayo yamevunjika kiasi siku mbili kabla ya baraza la mawaziri kukutana kujadili muswada wa taarifa ya umoja wa mataifa juu ya kuunda mahakama itakayoshughulika na mauaji ya mwaka jana ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.